KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 3, 2010

Walionusurika bado watafutwa Uganda



Uganda
Polisi wa Uganda wanaendelea kuwasaka walionusurika katika boti iliyopinduka kwenye ziwa Albert, huku maafisa wakisema wanahofia takriban watu 33 wamefariki dunia.

Boti hiyo ilipinduka wakati wa dhoruba iliyotokea Jumamosi usiku, maafa ya pili kutokea nchini humo katika kipindi cha wiki mbili.

Maafisa wanasema chombo hicho kilikuwa na kibali cha kubeba watu 40 lakini imekadiriwa ilikuwa na watu baina ya 50 na 90.

Watu 17 tu mpaka sasa wameokolewa na miili ya watu watano ndio iliyopatikana mpaka sasa.

Ajali za boti hutokea mara kwa mara katika maziwa ya Uganda.

'Kujaa pumoni'
Kamishna wa polisi wa eneo hilo Marcelino Wanithu alisema, " Tumepokea taarifa watu 33 wamezama."

Alisema, " Tunaamini huenda walikuwepo zaidi ya 50 kwenye boti hiyo, pamoja na mizigo. "Kulingana na uchunguzi uliofanyika hadi sasa, tunasema boti hiyo ilikuwa imejaa kupita kiasi."

Boti hiyo ilikuwa imebeba wafanyabiashara waliokuwa wamebeba bidhaa kutoka wilaya ya Hoima, upande wa kusini mwa ziwa Albert, kuelekea wilaya ya Nebbi, kaskazini mwa ziwa hilo.

Ziwa Albert, ziwa la saba kwa ukubwa barani Afrika, liko mpakani mwa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwezi uliopita, takriban watu 10 walifariki dunia katika ajali ya boti iliyotokea katika ziwa Victoria upande wa Uganda.

No comments:

Post a Comment