KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 3, 2010

Lebanon na Israel zafarakana

Lebanon na Israel zafarakana
Askari watatu wa Lebanon, afisa wa ngazi ya juu wa Israel na mwandishi wa habari wa Lebanon wameuawa katika majibizano ya risasi karibu na mpaka baina ya nchi hizo mbili.
Bendera ikipepea nchini Lebanon karibu na mpaka na Israel


Lebanon imedai kuwa walifyatua risasi baada ya kuona vikosi vya Israel vimeingia kwenye ardhi yao. Lakini Waisrael wamekanusha kuvuka mpaka.
Hii ni mara ya kwanza kwa mapambano makali kutokea tangu mwaka 2006 wakati wa mapambano baina ya Israel na wapiganaji wa kundi la Lebanon la Hizbullah.
Waziri mkuu wa Lebanon ameshutumu kitendo hicho cha uvamizi lakini Israel imejibu kwa kuionya kuwa itakiona cha moto ikiendelea kuleta fujo.

Askari wa Lebanon

Katika taarifa, Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri amesema kuwa hadhi ya taifa lake imekiukwa. Jeshi la Lebanon linasema kuwa askari wa jeshi la Israel walivuka mpaka na kuun'goa mti uliokuwa ukiwazuia kuona kijiji cha Adaysseh huko Lebanon.
Msemaji wa vikosi vya Lebanon amesema kuwa walifyatua risasi za kuwaonya askari hao na Israel ikajibu kwa kulipua makombora na kutuma helikopta.

Jeshi hilo limethibitishia BBC kuwa askari wake watatu waliuawa na wanne kujeruhiwa. Gazeti la Al Akhbar limethibitisha kifo cha mwandishi wao mmoja, Assaf Abu Rahhal.

No comments:

Post a Comment