KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 23, 2010

Waishi kwa hofu kwa kutishwa na paka


FAMILIA mbili tofauti ziishizo maeneo ya Kigogo Luhanga, wamekuwa wakiishi kwa hofu toka mwanzoni mwa wiki hii kutokana na kutishwa na paka wafikao katika nyumba hizo na kulia kwa zaidi masaa matatu na kupeleka kutishwa na hali hiyo inayowakabili
Wakazi hao ambao walionekana kukosa amani ya nafsi zao kutokana na kila ifikao majira ya saa saba za usiku paka hao wanaozidi wawili siku ya nne mfululizo wamekuwa wakifika maeneo hayo na kuanza kulia mithili ya binadamu na wamekuwa wakiwa hawana majibu paka hao walikuwa wa aina gani.

Walidai wakazi hao kuwa, hawana raha na imani zao kuwatoka ni kwanini paka hao walikuwa wakifika majira hayo kila siku na kulia mfululizo kwa sababu ambayo bado hawajaifahamu.

Walidai usiku wa kuamkia jana, familia hizo mbili walijitoa muhanga na kutoka nje ya nyumba zao na kuwafukuza paka hao ambapo hawakufanikiwa katika zoezi hilo na kila wakiwafukuza paka hao walikuwa hawakimbiii na kuwatazama hali ambayo inazidi kuwachanganya.

“Yaani hao paka wanalia mithili ya mtoto mchanga ameanguka, ni sikuya tatu sasa hatulali kabisa, sijui ni uchuro ama vipi” alihoji mmoja wa wanafamilia hao


"Hao paka wakija tena na kesho yaani [leo] tutafanya chini juu kukabiliana na dha hiyo" alidai

No comments:

Post a Comment