KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 23, 2010

TFDA yakamata maziwa bandia


MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imekamata makopo ya maziwa bandia ya watoto wachanga aina ya NAN 2 yanayotengenezwa na Kampuni ya Nestle ya Afrika Kusini.
TFDA imekamata makopo yapatayo 2260 ambayo yamewekwa nembo ya Nestle ambayo hayafai kwa matumizi ya watoto.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na tayari Mamlaka hiyo imeitarifu Nestle Tanzania kuhusiana na tatizo hilo na kuonekana maziwa hayo si ya kampuni hiyo na yamewekwa nembo hiyo na wahuni kwa lengo la kufanya biashara.

Hivyo TFDA imeutahadharisha umme kuwa makini kutokana na uhuni huo na kuwa makini katika ununuzi wa maziwa hayo.

Hata hivyo TFDA imesema maziwa hayo halisi yanatengenezwa nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment