KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 23, 2010

Akacha imani yake ya kidini


MSICHANA mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Sakina [22] amejikuta akikana imani yake kwa kuwa hakuwa tayari kusimama kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja kutokana na ofa iliyotolewa na mwajiri wake.
Msichana huyo mwajiriwa wa baa iitwayo nice iliyopo Mabibo, ilidaiwa kuwa alikana imani yake ya dini ya kiislamu kwa kuwa hakuwa tayari kusimama kwa muda kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, yeye na Sakina ni waajiriwa wa baa hiyo na mwajiri wao aliwataka wahudumu waislamu ambae anajiona atafunga mfungo wa mwezi wa Ramadhanai aliwataka wasimame ili waweze kutimiza amri hiyo takatifu ya Mwenyezi Mungu.

Hivyo kutokana na ofa hiyo ya mwajiri wao wasichana hao waliinua mikono juu na kumshukuru mwajiri wao na ambao walikuwa tayari aliwapa elfu ishirini ishirini kama kianzio cha kununua futari.

Alidai kilichowashangaza mwenzao huyo ambaye kila siku walikuwa wakimfahamu kama muislamu mwenzao alianza kukana imani hiyo na kuwaambia wenzake kuwa yeye ataendelea na kazi kama kawaida kwa kuwa yeye si muislamu.

Alidai, mwajiri wake huyo pia alipomuuliza kama atapumnzika alimjibu kwua yeye si muislamu ila jina lake ni la kislamu na kufafanua kwua baba yake ni kkristu mama yake ndio muislamu.

Kilidai chanzo hichao kuwa walisikitishwa na kitendo cha rafiki yao huyo kwa uchu na kuhis huenda akiwa mapumnziko atakosa pesa ndogondogo ambayo anipata kwa wateja wa kila siku

No comments:

Post a Comment