KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga, limetoka na kitu kipya kiitwacho ‘Sugu Nenda Bungeni’, ukiwa ni maalum kwa ajili ya kumpigia debe msanii huyo aliyechukua fomu ya kuwania Ubunge wa Mbeya mjini.
Wagosi wa Kaya wamedondosha kitu kipya kinachoitwa ‘Sugu Nenda Bungeni’,ili kumpigia debe msanii mkongwe wa Bongo Flava MR II aka "Sugu" aliyechukua fomu ya kuwania Ubunge wa Mbeya mjini kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza na mwandishi wa Nifahamishe.com jijini jana, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, alisema wameamua kuacha kazi zao ili kumfanyia kampeni Sugu kutokana na kuukubali uwezo wake.
Walisema kuwa wanamfahamu vilivyo Sugu alivyopigania haki na mtetezi wa wanyonge hivyo wanaamini akifika bungeni atakuwa na nafasi kubwa ya kuwatetea wananchi wa Mbeya.
“Tumeachia wimbo mpya wa ‘Sugu Nenda Bungeni’, tumeamua kumkampenia Sugu ili aingie bungeni tukiamini atawawakilisha vyema wananchi wa jimbo hilo,” alisema Mkoloni.
Alisema wanatarajia wimbo huo utawasaidia wananchi wa Jimbo hilo kumfahamu vyema Sugu na kumpitisha katika Chama chake na baadaye wamchague kuwa Mbunge wao, atakayewaletea maendeleo ya kweli.
No comments:
Post a Comment