KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 3, 2010

Baadhi ya vigogo CCM waanguka kura za maoni, uchaguzi watawaliwa na vu


JANA ilikuwa mshikemshike katika kila pembe ya nchi kwa kufanyika kwa uchaguzi wa kura za maoni za uteuzi wa madiwani na wabunge nchini kote.

Katika upigaji wa kura hizo baadhi ya vituo vilitawaliwa na vujo za aina yake baada ya wanachama wengine kuzuiliwa kupiga kura na huku wengine majina yao hayapo katika orodha ya upigaji kura hizo hali iliyofanya kura hizo ziingie dosari katika vituo hivyo.

WEngine walisimamishwa kupiga kura hizo zaidi ya masaa sita na kuleta vujo na mtafaruku ndani ya vituo hivyo.

Baadhi ya vituo vilivyoleta dosari ni kata ya Jangwani bada ya wajumbe kulalamikia kutoonekana kwa majina yao na kuzuiliwa kupiga kura.

Jimbo la Kigamboni walishindwa kupiga kura katika kata mpya ya Mianzini, baada ya kuzuiwa kupiga kura kwa kile walichoelezwa kuwa majina yao hayamo kwenye rejista ya uanachama.

Baadhi ya mawaziri amabao wameanguka katika maoni hayo akiwemo WEaziri wea Afya. Prof. David MWakyusa, John Malecela, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, Naibu Wziri wa Elimu, Mwantumu Mahiza, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Diodorus Kamala, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati hawa matokeo hayo yaliwabwaga bada ya matokeo hayo kutangazwa.

No comments:

Post a Comment