KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 3, 2010

'Mkuu wa polisi' Afrika Kusini ahukumiwa


Mahakama moja nchini Afrika Kusini imetoa hukumu ya kifungo cha miaka kumi na mitano gerezani kwa aliyekuwa mkuu wa polisi wa taifa Jackie Selebi, baada ya kukutwa na hatia kuhusiana na mashitaka ya ufisadi.


Jackie Selebi, aliyekuwa kamisha wa polisi Afrika Kusini


Selebi mwenye umri wa miaka 60 aliwahi kuwa rais wa polisi wa kimataifa (Interpol), alikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwa muuzaji wa dawa za kulevya.

Muuza dawa za kulevya ambaye pia alikutwa na hatia, Glenn Agliotti, alimlipa Selebi rand milioni 1.2, takriban dola laki moja na nusu, ili afumbie macho biashara hiyo.

Selebi ndio afisa wa ngazi ya juu wa kuteuliwa katika serikali ya Afrika Kusini, kukutwa na hatia ya ufisadi.


Jackie Selebi


Kamishna huyo wa zamani alikuwa anafahamiana vyema na watu katika serikali ya chama kinachotawala cha ANC.

Pia, Selebi aliwahi kuwa rais wa chama cha vijana cha ANC, mwakilishi wa Afrika Kusini katika Umoja wa Mataifa, na alikuwa mtu wa karibu wa rais wa zamani Thabo Mbeki.

Selebi, mwenye umri wa miaka 60 huenda akakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela.

Upande wa utetezi mahakamani umemuomba jaji kumpa kifungo cha nje na kumtoza faini.


Jackie Selebi


Lakini upande wa mashitaka umesema Selebi hajaonesha kusikitishwa na matendo yake.

Wakati kesi inasikiliza, mahakama ilielezwa jinsi Selebi alivyokuwa akitumia maelfu ya dola, fedha ambazo alikuwa akipewa na Agliotti.

Agliotti, ambaye alitoa ushahidi dhidi ya Selebi ili afutiwe mashitaka ya ufisadi, bado anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa uchimbaji madini.

No comments:

Post a Comment