KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 23, 2010

Wachimba migodi Chile hai baada ya siku 17


Wachimba migodi 33 waliokuwa wamekwama kwenye mgodi mmoja nchini Chile,wako hai wote hata baada ya kuwa huko kwa muda wa siku 17,Rais Sebastian Pinera amesema.

Waokoaji wamesikia kelele wakati walipotuma kifaa cha uchunguzi kwenye mgodi huo.

Kifaa hicho kilirudi na ujumbe wa karatasi ukisema: "wote sisi 33 tuko sawa."

Wanaume hao walikuwa wakifanya kazi kwenye shimo lenye urefu wa mita 700 katika mgodi wa San Jose,karibu na mji wa Copiapo, wakati wa jiwe lililokuwa juu yao liliporomoka.

Hadi Jumapili,hakukuwa na mawasiliano yoyote na wachimba migodi hao na matumaini ya kupatikana wakiwa hai yalikuwa yamefifia.

Lakini inaweza kuchukua miezi kadhaa kuchimba ili kuweza kuwaokoa wanaume hao.

No comments:

Post a Comment