KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 23, 2010

Tiba ya Ebola yapatikana


Wanasayansi wanaotengeneza dawa ya kutibu virusi vya ugonjwa wa ebola wameruhusiwa kujaribu dawa hiyo kwa binaadamu.

Serikali nchini Marekani imetoa ruhusa kwa majaribio kufanyika kwa wanaadamu baada ya dawa hiyo kugundulika kuwa tiba kwa tumbili.Ebola ni moja ya maradhi mabaya na yanaua.


Ugonjwa wa Ebola ni hatari zaidi kwa tumbili kuliko binaadamu.Wakipatikana na ugonjwa huu wanafariki dunia.

Lakini kwa majaribio ya dawa hii,asilimia sitini walitibiwa.Matumaini ni kwamba matokeo haya mazuri yatajitokeza au yawe bora zaidi wakati dawa hii itakapotumiwa kwa binaadamu.

Ebola imeua takriban watu elfu moja mia mbili tangu ilipogunduliwa katika miaka ya sabini nchini Zaire,sasa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Mara nyingi mlipuko wa ebola hutokea barani Afrika.

Ebola inaweza kuambukizwa kutokana na maji maji ya mwili.Dalili zake ni pamoja na kutapika huku walioathirika wakitoka damu pamoja na viungo muhimu vya mwili kushindwa kufanya kazi kabla hawajafariki dunia.Kutokana na kuwa na athari kubwa inahofiwa kuwa virusi vya ebola vinaweza kutumika kwa ugaidi.

Ufadhili wa utafiti ulitiliwa nguvu Marekani kufwatia mashambulio ya septemba kumi na moja mwaka 2001.

Dawa hii mpya imefanyiwa utafiti na idara ya utafiti ya jeshi la Marekani pamoja na kampuni nyengine binafsi ya AVI-BioPharma

No comments:

Post a Comment