KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 23, 2010

Sakata la paka mmoja afariki dunia


WAKAZI wa Kigogo Luhanga, ambao walikuwa wakikosa usingizi kwa ajili ya kukerwa na uliajia wa paka usiku kucha umeingia sura mpya baada ya mmoja kati ya wakazi hao kupoteza maisha ni usiku mmoja mara tu walivyofanya kampeni ya kuwaondosha paka hao.
Marehemu alitambulika kwa jina la Baraka Wilson [32] alifariki dunia usiku wa kuamikia leo baada ya kuuugua kwa muda mfupi.

Chanzo cha habari hii kilisema kuwa, paka hao waliendelea kuja usiku uliofuata na kupelekea siku nne mfululizo na baada ya hapo walijadiliana ni jinsi gani wataepukana na adha hiyo.

Hivyo kwa kuwa kero hiyo ilikuwa wakidai ni kubwa na inawanyima usingizi na kushikwa na woga, waliamua kuwakimbiza huku kila mmoja akifanya juhudi binafsi wengine wakiwarushia mawe bila mafanikio ndipo vijana wawili waliamua kulivavalia njuga suala hadi kuhakikisha paka hao hawarudi mahali hapo, waliamua kuwakimbiza kwa fimbo huku wakiwapiga kwa miti.

Kilidai chanzo hiki ambacho ni ndugu wa marehemu huyo kuwa, siku iliyofuata paka hao hawakuweza kurudi na kushukuru kuwa walifanikiwa katika kampeni hiyo.

Lakini walianza kupatwa na hofu baada ya siku iliyofuata ndugu yao huyo kuanza kuwaambia kuwa anajisikia vibaya na hataweza kufunga kwa kuwa kichwa kilikuwa kinamuuma kwelikweli, waliona ni kawaida na kupata huduma na kilivyozidi waliona walimpelekea hospitali na kurudi nyumbani huku akilalama na kichwa hicho.

Hivyo kufikia majira ya usiku jana ndugu yao huyo hali yake kila masaa yanavyozidi kwenda ndipo alizidi kulalamikia kichwa hicho na majira ya alfajiri leo ndugu yao aliweza kuaga dunia.

“Sasa hatujui sijui ni nini kilimmaliza kaka yetu? Tunahisi nip aka tu wale huenda walikwua na namna? Aliongezea kwa huruma.

Marehemu aliacha mchumba ambaye ilidaiwa angefunga nae ndoa mara tu baada ya mwezi mtukufu kumalizika.

Kwa habari zaidi juu ya tukio hili itawajia

No comments:

Post a Comment