KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, August 5, 2010
Viboko kwa kuvaa nguo za kike
Kundi la wavulana wa Kiislamu nchini Sudan limechapwa viboko baada ya kutuhumiwa kuvaa nguo za kike na kujiremba kama wanawake.
Ramani ya Sudan
Katika kutoa hukumu Mahakama imesema kuwa wavulana hao 19 wamevunja maadili ya Sudan yanayozingatiwa na raia wa nchi hiyo. Polisi waliwatia mbaroni kwenye tafrija walipokutwa wakicheza ngoma wakiwa wamevalia mavazi ya kike.
Watu hao hawakuwakilishwa mahakamani na hawakujitetea, baadhi wakificha uso mbele ya mamia ya watazamaji waliokuepo kushuhudia wakipigwa viboko.
Faini
Adhabu ya viboko 30 ilianza mara tu mahakama ya mjini Omdurman, karibu na Khartoum ilipopitisha uwamuzi wake.
Pamoja na viboko hivyo wametakiwa kulipa faini ya pauni za Sudan 1,000 sawa na dola za Marekani 400.
Wakili mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameliambia shirika la habari Reuters kuwa wavulana hao wameonewa katika maamuzi ya mahakama.
Mwanasheria huyo aliongezea kusema kuwa watu hao hawakupewa fursa ya sheria, ila wamehukumiwa na maoni ya watu na magazeti huku wanasheria wakiogopa kujitolea kuwatetea.
Magazeti yaliitaja tafrija ambako walikuwa wakicheza ngoma, kama harusi ya watu wa jinsia moja.
'Mila potofu'
Sudan ya kaskazini inaongozwa chini ya Sharia za Kiislamu na hivyo tabia ya watu wa jinsia moja kupendana ni haramu.
Sheria inayotawala mavazi yasiyostahili ilizuka mwaka uliopita kuhusu mwandishi habari wa kike aliyetuhumiwa kwa kuvaa suruwali.
Hata hivyo hukumu ilibadilishwa na kutozwa faini.
Tabia hiyo ya mapenzi ya jinsia moja haistahamiliki katika maeneo ya Sudan ya kusini, ambako watu wengi ni Wakristo au wengine ni wafuasi wa imani za kale.
Rais wa Sudan ya kusini, Salva Kiir alikiambia kituo cha Redio hivi karibuni kuwa tabia hiyo imeletwa tu kutoka nje.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment