KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 5, 2010

Kenya yaamua kuhusu mabadilko ya katiba


Matokeo ya mapema ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya nchini Kenya yanaonyesha kuwa katiba hiyo imeungwa mkono kwa wingi wa kura.

Baadhi ya mapendekezo kwenye katiba hiyo ni kupunguza mamlaka ya rais, kulinda haki za kibinadam za wakenya pamoja na kubuni sera mpya ya umiliki wa ardhi.

Hata hivyo katika maeneo ya mkoa wa Rift Valley ambako ghasia za baada ya uchaguzi ziliathiri wengi, wengi walipiga kura ya kupinga katiba hiyo wakisema kuwa itachochea vurugu za kisiasa katika eneo hilo.

Kura hiyo imefanyika bila vurugu lolote ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo ghasia zilizuka kufuatia na kkuwaacha watu elfu moja miatano wakiwa wamefariki na wengine takriban nusu milioni bila makao.

No comments:

Post a Comment