KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 23, 2010

Aliyetaka kuuza albino mzimamzima jela miaka 17


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza, imemuhukumu kifungo cha miaka 17 jela, au faini ya shilingi milioni 80 Nathan Mtei (28) baada ya kupatikana na hatia ya kumsafirisha na kumtorosha mlemavu wa ngozi kwa lengo la kumuua.


Hukumu hiyo ilitolea jana mbele ya Hakimu Mkazi, Angelo Rumisha, huku shauri hilo likiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, David Kakwaya.

Awali akisoma hati ya mashitaka kabla ya hukumu hiyo, ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo Agosti 15 mwaka huu, mkoani Mwanza kwa lengo la kudhamiria kumuua Robinson Mtwana (20) [albino] ambaye ni raia mwenzake wa nchini Kenya

Kakwaya alidai kuwa, kitendo cha kusafirisha binadamu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni kosa la kisheria na ni tendo la kinyama na kuiomba mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo .

Kabla ya hakimu kutoa hukumu alimtaka mshitakiwa ajitetee ili asimpe adhabu kali na kuiomba mahakdfama kamda ifuat avyo.

“Naomba mahakama iruhusu kesi hiyo ikasomewe Kenya” pia naomba mahakama inisamehe inisamehe kwa kuwa anahisi mganga wa kienyeji alichangia kumshawishi kutenda makosa hayo.

ALiongeza kwa kuiomba mahakama kuwa “ nina familia ambayo inanitegemea”

Hivyo baada ya Kwakwaya kumaliza Hakimu alitoa adhabu kwa mshitakiwa ambapo alisema kwa kosa la kwanza atatumikia miaka tisa jela au kulipa faini ya Shilingi milioni 80 na kwa kosa la pili atatumikia jela miaka minane.

Na kuongeza kuwa endapo mshitakiwa atalipa faini adhabu hiyo itabadilika .

Pia Hakimu alimpa siku 45 mshitakwia huyo kukata rufaa ndani ya mahakamda kuu endapo hajaridhishwa na hukumu iliyotolewa dhidi yake.

No comments:

Post a Comment