KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 30, 2010

Sakata la kugombania maiti bado tata

SAKATA la kugombea mwili wa marehemu, Onesmo Kazahura bado haijafahamika mwili huo utazikwa wapi baada ya shauri hilo kufikishwa katika mahakamani ya Kinondoni jana.
Sakata hilo limehamia mahakamani baada ya mke wa marehemu kuushitaki uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuzuiliwa kuchukua maiti hiyo kwa ajili ya mazishi.

Hatua ya mke huyo aliyefahamika kwa jina la Joyce Owenya kutinga mahakamani, ni baada ya ndugu a marehemu kutaka kuchukua mwili huo na kwnda kuuzika Mkoani Kagera nay eye anahitaji azike mwili wa mumewe Dar es Salaam.


Akisikiliza hsauri hilo mahakamani, Hakimu Mkazi Suzanne Kihawa, alisema shauri hilo litasikilizwa na kutolewa uamuzi Jumatatu ya wiki ijayo na kwa kuwa leo atasikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Muhimbili .

Kazaula, alifariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita hospitalini hapo ambako alikuwa akiugua maradhi ya tumbo na mwili huo ulitakiwa uzikwe Agosti 24 mwaka huu, katika makaburi ya Kinondoni ilishindidka baada ya ndugu hao kuzuia kibali cha maazishi na kuutaka mwili huo ukazikwe Bukoba

No comments:

Post a Comment