KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 30, 2010

Mahakamani kwa kujipatia ngono kwa njia ya madawa ya kulevyaSHABANI MJEMA [30] Mkazi wa Kimara Rombo jijini Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akikabiliwa na tuhuma za kuwalewesha wanawake wawili kwa dawa za kulevya kisha kuwaingilia kimwili.
Mtuhumiwa huyo alipandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka mawili na kusomewa mashitaka hayo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Braina John mbele ya Hakimu Benadict Beda.

John alidai kuwa, mtuhumiwa alifanya kosa hilo Agosti 11 mwaka huu, katika eneo la Manzese Tip Top alimuingilia kimwili mwanamke wa miaka 30 jina kapuni kabla ya kutenda hivyo alidai mshitakiwa alimlewesha kwa dawa za kulevya.

John alidai kuwa, baada ya kumuingilia kimwili bila ridhaa yake, mshitakiwa alimuibia mwanamke huyo pete ya dhahabu yenye thamani ya Shiliomngi 250,000 na simu yenye thamani ya Shilingi 75,000 kwa pamoja.

Katika shtaka la pili, mshitakiwa huyo alisomewa shtaka hilo la aina hiyo kwa hakimu Enediana Makabwa kwa kudaiwa kumuingilia kimwili mwanamke mwingine tofauti na huyo

Ilidai kuwa, Agosti 10 mwaka huu, katika eneo la Shekilango, mshitakiwa alimlewesha mwanwamke huyo kwa dawa za kulevya na kumuingilia kimwili mwanamke huyo bila kujitambua na alifanikiwa kumuibia mwanamke huyo mikufu miwili ya dhahabu yenye thamani ya Shilingi 52,000, pete mbili za dhahabu zenye thamani ya shilingi 250,000 na simu ya mkononi yenye thamani ya shilingi elfu 63,000.

AHata hivyo mshitakiwa huyo alikana m shitaka yote mawili katika vizimba tofauti na ali rudishwa rumande kwa kukosa wadhamini na kesi hiyo itatajwa tena Septemba 9 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment