MEGUNDULIKA baadhi ya makahaba hutumia kuvaa vazi aina ya baibui na kisha kuelekea nalo kuendesha shuhguli zao za kila siku ndani ya mwezi huu mtukufu wa R amadhani.
Hali hiyo ambayo iliwashangaza wanahabari wa NIFAHAMISHE kuona baadhi ya makahaba hao kutinga vazi hilo na kusimama nalo katika maeneo yao ya biashara hiyo.
Hayo yaligundulika katika tafiti zilizofanywa na wanahabari hao na kubaini kuwa mwezi huu huheshimiwa hata na makahaba wa jijini kwa kuvaa vazi hilo wanapoelekea sehemu zao za kazi.
Katika tafiti hiyo nifahamishe ilibahatika kuona wadada watatu tofauti wanaoendesha shughuli hiyo wametinga vazi hilo kisha wanapofika maeneo yao ya kazi kuvua vazi hilo tayari kwa kusubiri wateja.
Majira ya saa 2 na nusu juzi, majira ya saa 4 kasorobo jana, wanahabari hao katika harakati za kusaka habari waliwaona wadada hao huku mmoja wao ametinga vazi hilo na kulinyatia gari hilo wakidhani ni wateja wao wa kila siku.
Katika kuhakiki walipomuuliza ni kwa nini alivaa vazi hilo alidai kuwa “ ndio ninafika huwa nabadilisha msijali” walipomuuliza zaidi ni kwanini hakuja moja kwa moja na mavazi ambayo yalikuwa yanazoeleka ya nusu uchi alidai” jamani si mnajua huu ni mwezi mtukufu lazima tujiheshimu” alidai
Mbali na eneo hilo pia alionekana mwanadada mwingine ambaye yeye alionekana kuketi na vazi hilo kama si muhusika katika biashara
No comments:
Post a Comment