KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 3, 2010

Rubani aliyetekwa nyara DRC aachiwa huru



Hatimae rubani aliyetekwa nyara kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameachiwa huru. Rubani huyo raia wa Ufilipino alitekwa nyara mwezi uliopita baada ya ndege yake kutua katika eneo moja linalomilikiwa na waasi wa Kihutu FDLR.

Kwa mujibu wa taarifa ya maafisa Kaskazini Mashariki mwa Congo, rubani huyo aliachiwa huru baada ya kasisi mmoja wa kikatoliki mwenyeji wa Walikale kushauriana na watekaji nyara . Rubani huyo pamoja na wenzake wanne akiwemo mtoto walitekwa nyara pale ndege yao ilipotua eneo la Walikale.

Mbunge wa eneo hilo Sabin Binti Muhima ameewalaumu waasi wa Ki-Hutu kutoka kundi la FDLR kwa kuhusika na utekaji nyara huo.

Maafisa wamekanusha kwamba watekaji nyara walilipwa kikombozi kama sharti la kuachia mateka aliysalia, japo kuna duru kamba watekaji nyara hao walitaka kikombozi na dola laki mbini unusu.

Waasi wa FDLR wamekuwa wakiendesha harakati zao kaskazini mashariki mwa Congo baada ya kuhama ngome zao za zamani walipokabiliwa na operesheni ya majeshi ya Rwanda wakishirikiana na wenzao kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waasi hao wa Ki-Hutu wamelaumiwa kwa kutekeleza mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka wa 1994 na kisha kukimbilia mashariki mwa Congo.

No comments:

Post a Comment