KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, August 3, 2010
Pakistan yatoa ombi jipya la msaada
Takwimu mpya za umoja wa mataifa zimeonyesha hali mbaya zaidi ya uharibifu uliotokea nchini Pakistan kutokana na mafuriko, ambayo yamesemekana kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka themanini.
Wanaoendesha shughuli za uokozi katika mafuriko yanayokumba Pakistan kwa sasa wanatarajiwa kuwafikia watu elfu ishirini na saba ambao wangali wamekwama katika maeneo yaliyofurika maji kaskazini mwa nchi.
Kulingana na mashirika ya misaada vijiji kadhaa vilizama katika mafuriko hayo yanayosemekana kuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miaka themanini.
Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa mataifa, Unicef, limekadiria watu milioni tatu wameathirika kutokana na mafuriko hayo huku takwimu zikionyesha kuwa kati ya watu mianane na elfu moja miatano wamefariki.
Mahitaji muhimu kwa sasa kulingana na umoja huo, ni mahema, chakula na maji safi ya kunywa pamoja na huduma nyinginezo za afya.
Afisaa mwandamizi wa shirika la afya duniani nchini Pakistan, Ahmed Farah Shadoul, amesema angalau hakuna visa vyovyote vya kipindupindu vimeripotiwa ingawa kuna hatar ya kuzuka ugonjwa huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment