KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 31, 2010

Ramli ya Joseph ilisema hivi!HUU ni mfululizo wa habari ambayo ilishaandikwa katika mtandao huu wiki iliyopita, kuhusiana na kufatilia mfululizo wa sakata la Joseph aliyekuwa akipatiwa matibabu kwa maganga wa kienyeji Chamanzi.
NIFAHAMISHE imebainika na imejuzwa kuwa, ramli iliyopatikana kwa mganga huyo kutokana na maradhi ambayo yalikuwa yakimsumbua Joseph ni yalikuwa ni mkono wa mtu.

Ramli hiyo ilisema” Joseph ndiye alitakiwa apoteze maisha na badala yake kifo hicho kikamkuta mwenzie aliyeshirikiana nae kwa kuwa alikuwa hana kinga yoyote” ilidaiwa

“ Aisee ni siri lakini tunashukuru mgonjwa anaendela vizuri laini tungechelewa kidogo tungemkosa Joseph, kumbe alitupiwa jini’ wale paka kumbe walikuwa si wa heri, alidai ndugu huyo
Mganga alisema kuwa tungechelewa kidogo tungemkosa kutokana na hali yake, kwa kuwa alikuwa mzito yaani alikuwa na kinga ndio mana kitu alichotupiwa hakikummaliza mapema” binadamu wabaya aliendelea kudai ndugu huyo

Hivyo ndiyo ramli ambayo wasomaji mliahidiwa juhudi binafsi zitafanyika na kuletewa ramli hiyo.

Joseph anaendelea vizuri na imedaiwa leo ameanza kwenda kazini kwake anapopata riziki yake kila siku

Hata hivyo ilibainika kuwa Joseph alikuwa na bifu na familia moja iishiyo maeneo ya Mburahati baada ya kusitisha uchumba kwa binti mmoja aliyetambulika kwa jina la Grace ambaye alidumu nae kwenye uchumba huo zaidi ya miaka mitatu.

Na kudaiwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu Joseph alimvalisha pete ya uchumba msichana mwingine na tayari ameshakwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti huyo na kumuacha mchumba wake wa awali.

No comments:

Post a Comment