KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 31, 2010

7 papohapo, wengine majeruhi ajalini- Mabibo


WATU wanne waliokuwa wakipata huduma katika mgahawa mmoja maeneo ya Mabibo Mwisho Stand wamefariki dunia papohapo baada ya gari aina ya Toyota Surf T 365 BHS kuacha njia na kuingia ndani humo.

Watu hao akiwemo na mkaanga chips wa mgawhawa huo na wengine watatu ni wateja waliokuwa wakipatiwa huduma ndani ya mgahawa huo waliweza kupoteza maisha.

Wengine ni wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa wakiendesha shughuli zao maeneo hayo wakiwemo mafundi baiskeli, maduka na wengine waliweza kujeruhiwa vibaya baada ya gari hilo kuja mwendo kasi kupita kiasi na kupoteza maisha ya watu hao.

Ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea jana, majira ya adhuhuri baada ya gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese kuacha njia na kushindwa kukata kona kali iliyopo maeneo hayo na kuvamia watu hao na hatima yake kuingia ndani ya mgahawa huo.

Baada ya kutokea ajali hiyo mtu huyo aliweza kukimbia na kuacha watoto aliokuwa nao ndani ya gari hilo na kutoweka na hakujuliakan alikimbili wapi wka wakati ule.

Hata hivyo ilidaiwa kuwa mtu huyo alikuwa akikimbizwa baada ya kugonga mtu maeneo ya Urafiki ktika barabara ya Morogoro na katika juhudi za kukimbia aliweza kuiongia barabara hiyo ya Mabibo naq hatima yake alipofika maeneo hayo hakutambua kama kulikuwa na kona hiyo na kuweza kusababisha vifo hivyo na majeruhi kadhaa na kuacha eneo hilo lilizizima kwa huzuni baada ya maisha ya watu hao kupoteza maisha bila hatia.

Majeruhi wa tukio hilo wamekimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na gari hilo lipo katika kiutuo cha polisi cha Magomeni.

No comments:

Post a Comment