KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Raia wa Israel aliyefungwa Libya aachiwa


Mtu mmoja kutoka Israel, aliyeshikiliwa Libya tangu mwezi Machi kwa kushukiwa kufanya shughuli za ujasusi, ameachiwa huru.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa Rafael Hadad alipelekwa Vienna ambapo alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman.

Bw Lieberman alihusishwa katika majadiliano juu ya kuachiliwa huru kwa Bw Hadad.

Hakuna kauli yeyote iliyotolewa kuhusu kesi hiyo na serikali ya Libya.

Maafisa wa Israel walisema, Bw Hadad alikamatwa wakati akipiga picha maeneo ya kumbukumu ya Israel nchini Libya.

Bw Hadad aliye na uraia pacha wa Tunisia na Israel, anaripotiwa kuwepo Libya kwa niaba ya kundi la Israel linaloshughulika na kuhifadhi historia ya jumuiya ya Kiyahudi iliyotoweka Libya.

Alikuwa hajulikani alipo mpaka Jumapili, wakati maafisa wa Israel walipotangaza kuwa aliachiwa huru na mamlaka ya Libya baada ya majadiliano ya muda mrefu.

Jeshi la Israel liliamuru kesi hiyo iwe siri kwa kuhofia usalama wa Bw Hadad.

Libya na Israel kimsingi kama wako vitani. Raia wa Israel wamepigwa marufuku kutembelea Libya. Bw Hadad alikuwa akisafiri na pasipoti yake ya Tunisia alipokamatwa.

No comments:

Post a Comment