KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Farrow asema "Taylor katuma almasi'

Muigizaji wa kike Mia Farrow ametoa ushahidi kuwa mwanamitindo Naomi Campbell alisema kapata "almasi kubwa" kutoka kwa watu waliotumwa na aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor.

Ushahidi uliotolewa na Bi Farrow unapingana moja kwa moja na ule wa Bi Campbell wa kuwa alipokea mawe mawili au matatu na hakujua nani alimtumia.

Kumhusisha Bw Taylor na "almasi haramu zinazotumika kugharamia vita" ni muhimu sana kwa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ya uhalifu wa kivita huko the Hague.

Bw Taylor amekana kuhusika na makosa yote 11.

Anatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone, ikiwemo kutumia almasi kufadhili waasi.


Mazungumzo wakati wa kifungua kinywa
Akitoa ushahidi katika mahakama maalum ya Sierra Leone wiki iliyopita huko Uholanzi, Bi Campbell alisema alipewa "mawe machafu" baada ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela mwaka 1997.


Naomi Campbell
Lakini alisema hakujua kama ni almasi na hakujua zilitoka kwa nani.

Hata hivyo, Bi Farrow ameiambia mahakama kuwa Bi Campbell alipokwenda kuungana na wenzake kwa kifungua kinywa siku ya pili asubuhi, alianza kuzungumza hata kabla hajakaa chini.

Bi Farrow alisema, " Ninachokumbuka ni Naomi Campbell alisema 'Mungu wangu ..... jana niliamshwa usiku baada ya kusikia mtu anagonga mlangoni kwangu na wanaume wawili walitumwa na Charles Taylor na amenipa...almasi kubwa.'

Wiki iliyopita Bi Campbell aliiambia mahakama kuwa alimkabidhi mawe hayo Jeremy Ratcliffe wa mfuko wa kusaidia watoto wa Nelson Mandela (NMCF) asubuhi iliyofuata, kwasababu alitaka mawe hayo yasaidie kwenye masuala ya misaada.

Bw Ratcliffe ameshakabidhi madini hayo kwa polisi, na siku ya Jumapili wamethibitisha mawe hayo ni almasi ya kweli.

No comments:

Post a Comment