KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, August 9, 2010
Rwanda wamchagua rais
Asubuhi hii Raia wa Rwanda wanashiriki katika uchaguzi wa rais kwa mara ya pili tangu yalipofanyika mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994.
Kuna wapinzani watatu wanaoshindana na rais wa sasa Paul Kagame kwenye uchaguzi huo, lakini rais Kagame anatarajiwa kupata ushindi.
Mwandishi wa BBC mjini Kigali anasema kuwa vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema na raia walionekana wakielekea kwenye vituo hivyo. Wachunguzi 200 wa kimataifa wako nchini humo kusimamia uchaguzi huo.
Bwana Kagame anaongoza kundi la waasi wa kitutsi Rwandan Patriotic Front (RPF) na anasifiwa kumaliza mauji ya kimbari na kuimarisha usalama na ukuaji wa uchumi.
Lakini wakosoaji wake wanamshutumu kuhujumu demokrasia na kuubana upinzani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment