Mwanafunzi mmoja wa sekondari amenusurika maisha yake baada ya kunywa sumu ya panya akijaribu kujiua kwa kile alichosema ameichoka dunia, katika tukio jingine mwanaume mmoja amefariki baada ya kujinyonga kwa kamba ya katani.
Scolastica Uloga [16] asomae kidato cha kwanza, katika shule ya sekondari Malamba Mawili Mbezi, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, akikabiliwa na shitaka la kujaribu kujiua na sumu ya panya kwa kile alichodai amechoshwa na dunia.
Mwanafunzi huyo amesomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Suzan Kihawa, huku upande wa mashitaka ukiongozwa na na Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi, Nassoro Sisiwaya.
Sisiwaya alidai kuwa, Julai 17, mwaka huu, majira yasiyofahamika, mshitakiwa alijaribu kujiua kwa kutumia sumu ya panya kwa kile alichodai kuwa amechoshwa na dunia.
Sisiwaya alidai mwanafunzi huyo mkazi wa Kigogo aliiambia mahakama kuwa hata wakimuachia dhamira yake iko palepale na kutekeleza hayo na lazima atakunywa sumu kwa mara nyingine na ili aweze kondoka duniani hapa.
Kesi hiyo itatajwa tena, Agosti 10, mwaka huu.
Katika tukio jingine la aina hiyo, KASHINDE [25-30], mkazi wa Mivumoni, amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aina ya katani.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, amesema tukio hilo lilitokea jana saa 3 asubuhi, huko,mtaa wa Mivumoni Wazo Hill Dar es Salaam.
Kalinga alithibitisha na kusema, marehemu huyo alikutwa akiwa ameshafariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba nene ya katani aliyoitundika juu ya mwembe jirani na nyumba anayoishi.
Chanzo cha kujinyonga kwake bado hakijafahamika na maiti ilichukuliwa na kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.
No comments:
Post a Comment