KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, August 5, 2010

'Tusiwadharau Wapinzani' - Kikwete


Rais Kikwete, amewakumbusha wanachama wenzake na wafuasi wa chama hicho, kuacha kudharau wapinzani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Rais Kikwete aliyasema hayo baada ya vigogo wapatao zaidi ya ishirini waliokuwa wakijiamini sana kuangushwa kuangushwa katika kura za maoni nchini kote.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana jijini Dar es Salaam, alisema ni lazima chama hicho kijipange kivita bila dharau, ili kishinde.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, CCM ina changamoto kubwa kutokana na upande wa Upinzani kuweka watu wapya na makini.

Alisema mwaka huu si wa chama hicho kubweteka na kudhani kuwa kitashinda kirahisi. “Jamani tujitahidi, la sivyo tutaadhirika, majuto siku zote ni mjukuu, tujitahdi katika kampeni jamani, mdharau mwiba guu huota tende, tutumie maarifa yetu yote.” alisisitiza Kikwete huku akiwa na hofu ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment