KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, August 25, 2010

Matatani kwa kujaribu kulawiti


MWANAUME mmoja aliyefahamika kwa jina la Sylivester [40], mkazi wa Dodoma vijijini, amejikuta yupo kwenye wakati mgumu baada ya kugundulika alikuwa katika jaribio la kulawiti mtoto wa kiume mwenye miaka 10.
Sylivester anakabiliwa na tuhuma hizo na jamaa yake ambaye anaishi nae kwa sasa jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo anatuhumiwa na jamaa yake ambaye alifikia nyumbani kwake akitokea mkoani Dodoma kwa ajili ya kuja kutafuta kazi jijini humu.

Inadaiwa kuwa mwenyeji wake huyo anamtuhumu sylivester kwa kutaka kumlawiti mtoto wake kwa kuwa mtoto huyo alimdokeza baba yake vitendo alivyokuwa akimfanyia wakati wazazi wake hao hawapo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kuulizwa kuhusiana na jaribio hilo, imedaiwa alitoweka nyumbani hapo na hakujulikana amekimbilia wapi ili hali yu mgeni jijini humu.

Inadaiwa kuwa baba wa mzazi huyo anamtafuta kwa udi na uvumba kumsaka jamaa yake huyo kwa jamaa zake wengine waishio jijini humo ili aweze kumpatia nauli arudi mkoani Dodoma alikotoka kwa kuwa alishamuona anaweza akamuharibia watoto wake.

No comments:

Post a Comment