KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, August 25, 2010

Hatma ya Muro Agosti 27


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, inatarajia kutoa uamuzi kwa kesi inayomkabili mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Taifa (TBC1), Jerry Murro, na wenzake, kama atakuwa na kesi ya kujibu ama kuachiwa huru.
Jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Gabrile Milumbe alidai kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka umekamilika hivyo mahakama itatoa uamuzi huo Agosti 27 kama watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu au la.

Muro na wenzake wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya shilingi Milioni 10 na kufikishwa katika mahakamda hiyo.

No comments:

Post a Comment