Wakati Bongo watu wakilalamika foleni za magari kusababisha watu wapoteze masaa machache barabarani, Nchini China watu wanakabiliwa na foleni ya ajabu ya magari ambapo kutoka mji mmoja hadi mwingine foleni inatumia siku tisa.
Fikiria foleni ya siku tisa barabarani, gari likitambaa kwa mwendo wa jongoo.
Hali hiyo inapatikana nchini China katika barabara kuu inayoingia mjini Beijing.
Foleni hiyo inatesa watu kwa umbali wa kilomita 100 ambapo magari yanatumia siku tisa kukatiza eneo hilo lenye foleni ndefu ya magari.
Ili kusogeza muda, madereva wa magari makubwa wamekuwa wakicheza karata ndani ya magari yao.
No comments:
Post a Comment