KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, August 30, 2010
Chadema yamuwekea pingamizi Kikwete
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemuwekea pingamizi mgombea urais kupitia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete kwa kuwa ametengua kanuni za sheria za uchaguzi na kudai ametoa rushwa kwa wapiga kura wakati wa kampeni.
Hayo yameongewa jana, na mgombea urais wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa na wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi za makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam .
Dk. Slaa alisema kuwa Rais Kikwete ametoa rushwa kwa wapiga kura kwa kutangaza kuongeza kima cha chini cha mishahara kw wafanyakazi katika uzinduzi wa kampeni zake ikiwa Bunge haijaidhinisha nyongeza hiyo.
Alisema kitendo hicho cha Kikwete kutangaza kuongeza mishahara hadharani katika kampeni ni kuomba rushwa wka wapiga na kudai sheria ifate mkondo wake.
Pia Dk Slaa aliongeza kwa kumtuhumu kuwa, Kikwete alizungumzia masuala ya kiserikali katika kampeni hizo hali ambayo alidai ni matumizi mabaya ya madaraka kwa kuwa yumo ndani ya chama tawala naw eapig a kura wanaweza wakashawishika
Na kusema Kikwete alitumia kampeni hizo kuwatangaza wagombea wa CCM waliopita bila pingamizi katiika majimbo hali aliyodai ni kinyume na kanuni za sheria za uchaguzis wa nchi.
Slaa teyari ameshawaagiza wanasheria wa chamda hicho kushughuliki kuweka pingamizi dhidi ya mgombea huyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment