Pakistan imetoa tahadhari wakati mafuriko yaliyosababisha maafa makubwa maeneo ya kaskazini magharibi yanaelekea jimbo la Sindh, ambalo ni kitovu cha kilimo nchini humo.
Serikali imewahamisha maelfu ya watu wanaoishi karibu na Mto Indus, wakati mamia ya watu wengine wakizingirwa na maji mengi yaliyotokana na mafuriko.
Waziri Mkuu Raza Yousuf Gilani ametoa wito kwa jamii ya kimatifa kutoa msaada wa dharura.
Mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea mkoani humo kwa muda wa miaka 80 yamewaua watu wasiopungua 1,600 na kuwaathiri wengine takriban millioni 14 million.
Maafisa wanasema nyumba 650,000 ,ardhi yenye mazao hektari 557,000 zimeharibiwa na mafuriko, huku ngombe zaidi ya 10,000 wakiangamia.
Ndege zasitisha kazi
Idara ya hali ya hewa ya Pakistan imetabiri mvua nyingine kubwa katika mkoa ulioathirika vibaya wa Khyber-Pakhtunkhwa, kaskazini-magharibi.
Ndege zote za helicopter katika eneo la kaskazini magharibi ambazo zilikuwa zinatumika kusambaza misaada na kuwaokoa manusura zimesitisha kazi kutokana na hali mbaya ya hewa, kulingana na Amal Masud kutoka Idara ya ya Taifa ya inayosimamia Majanga.
Waziri Mkuu Gilani alisema mafuriko hayo ni mabaya zaidi kuwahi kutokea Pakistan kwa miaka 63 katika historia ya Pakistan.
Rais apinga kukatisha ziara yake
Baadhi ya watu wanamtaka Rais Asif Ali Zardari kukatisha ziara yake ya nchi za nje ili kusimamia juhudi za kuwasaidia waathiriwa.
Lakini Rais amepinga shutma hizo.
Katika mahojiano na BBC, Bw Zardari alisema waziri mkuu ndiye anayesimamia operesheni hizo, na yeye binafsi anapatiwa taarifa kuhusu hali ilivyo kila wakati.Rais Zardari alisema kuwa alihakikishiwa misaada kutoka mataifa aliyozuru, kama vile Falme za Kiarabu, Ufaransa na Uingereza.
Hapo awali, afisa katika Umoja wa Mataifa, alisema baadhi ya raia wa Pakistan watalazimika kutegemea chakula cha msaada katika msimu huu.
No comments:
Post a Comment