KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Fidel Castro ahutubia bunge Cuba

Kiongozi wa zamani wa Cuba, Fidel Castro, ameonya kuhusu hatari ya kuzuka kwa vita vya nuclear, katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge la taifa baada ya miaka minne.

Shangwe na vigelegele vilitawala bunge, huku wajumbe wakimtakia maisha marefu Fidel Castro wakati akiingia kwenye kikao.

Castro ambaye anatimiza miaka 84 wiki ijayo, alipanda pole pole kwenye jukwaa, akisaidiwa na msaidizi wake.

Alivalia mavazi yake ya kijeshi yenye rangi ya kijani.

Mara ya mwisho kulihutubia bunge ilikuwa miaka minne iliyopita, mwezi mmoja kabla ya kufanyiwa upasuaji mkubwa na kumkabidhi madaraka mdogo wake Raul.
Fidel Castro aliitisha mkutano huo kuzungumzia hofu aliyonayo kuwa Marekani inataka kuzivamia Iran na Korea ya Kaskazini, na kuongeza kuwa hatua hiyo itaifanya dunia iangamie kwa silaha za nuclear.

Sauti yake ilikuwa na nguvu, zaidi ya ilivyokuwa wakati wowote tangu aonekane tena hadharani mwezi uliopita.

Katika hotuba yake hakugusia chochote kuhusu siasa za Cuba wala mageuzi yanayofanywa na mdogo wake.





















Inaonekana kuwa hotuba hiyo ilikuwa na ujumbe kuhusu maisha ya wanadamu, na kuinusuru dunia kutokana na maangamizi ya silaha za nuclear.

No comments:

Post a Comment