KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Lipumba achukua fomu ya Urais

MGOMBEA wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, jana alichukua fomu za kuwania kiti hicho katika ofisi za Tume ya Tifa ya Uchaguzi.

Lipumba alisindikizwa na wafuasi wa chama hicho kwa shangwe na vifijo na baadae kulelekea ktika ofisi za makao ya chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

Lipumba aliweza kuongozana na Katibu Mkuu wa chamda hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Machano Khamis na wajumbe wengine wa Baraza Kuu la CUF Taifa.

Akiwa katika ofisi hizo, Lipumba aliweza kuwaambia waandishi wa habari kuwa endapo akichaguliwa na kuwa rais ataleta mabadiliko makubwa nchini na kuondoa umaskini unaowakabili Watanzania wealio wengi.

Alisema umasikini huo ambao unadumu kwa watanzania ni kutokana na laana inayotokana na udhalimu unaofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema, CUF kuelekea Uchaguzi Mkuu wamejipanga kutumia sera na dira ya mabadiliko itakayowaamsha Watanzania na kuweza kutambua mafisadi wanavyo hatarisha uchumi wa taifa.

Aliongeza kuwa wakiingia madarakani, watasimamia ukuzaji wa uchumi na kuboresha sekta ya wakulima, ajira na kudhibiti mfumko wa bei kwa bidhaa za ndani unaozuka kila kukicha bila mpangilio maalum.

No comments:

Post a Comment