KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

wanafunzi 18 wafa maji -Mwanza


WANAFUNZI 18 wamefariki dunia, baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kwenda shuleni kuzama Ziwa Victoria
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Simon Sirro alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 1:30 asubuhi wakati wanafunzi hao walikuwa wakienda shuleni kwa kutumia mtumbwi huo

Wanafunzi hao walikuwa wakisoma shule ya msingi Lukumbi, wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Alisema, chanzo cha ajali hiyo ni watu walijazana kwenye mtumbwi huo.

Hadi kufika jana jioni, Sirro alisema tayari miili ya watoto wanne ilishapatikana ikielea majini na juhudi zaidi zinaendela kupata miili ya weanafunzi walisalia

Miili ya wanafunzi iliyopatikana ni Judica Ajemy, Jassi Omary, Dainess Scolla, na David Kizingamila.

No comments:

Post a Comment