KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Chatu atia hofu wakazi wa Keko

Chatu atia hofu wakazi wa Keko
WAKAZI wa Keko na Vitongoji vyake wamekuwa hawana amani baada ya ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyopo maeneo hayo kuwatangazia kuwa kuna chatu ametoweka na kuwataka wakazi hao wawe waangalifu katika shuguli zao za kila siku.
Tangazo hilo lilitolewa na wafanyakazi wa wizara hiyo baada ya kutoonekanea kwa chatu huyo aliyehifadhiwa katika moja ya majengo hayo.
Tangazo hilo lilisema kuwa, chatu huyo alihifadhiwa na kutakiwa asafirishwa kuelekea katika maonyesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma haonekani mahali alikohifadhiwa.
Iliendelea kuwa mwanzoni alihifadhiwa katika moja ya chumba wizarani hapo kililochojulikana kama IVORY ROOM, na walihisi atakuwa amejificha sehemu zenye giza na mrundikano wa takataka.
Taarifa hiyo ilisema kuwa yeyote atakayepata taarifa za kuonekana kwa chatu huyo atoe taarifa kwa Mkuu wa Kanda Kikosi dhidi ya ujangili Kanda ya Mashariki.

Hata hivyo Nifahamishe ilipata fursa ya kuongea na wakazi wawili watatu wa maeneo hayo na wakazi hao kudai kuwa hawana raha na maisha toka kutolewa kwa tangazo hilo juzi, na kukosa amani kabisa.

Wengine walidai kuwa wanaogopa kwenda hata msalani kwa hofu ya kukutana na chatu huyo huku wazazi wengine wakiwakataza watoto wao hata kwenda kucheza nje ya nyumba zao kwa hofu ya kukutana na chatu huyo.

Hata hivyo mmoja wa mkazi wa maeneo hayo alidai kuwa, jana wakati watoto wakicheza mpira walimuona chatu huyo na walikimbia kwenda kuwaeleza watu wazima na waliporudi hawakumuona tena.

No comments:

Post a Comment