KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Libya yakubali kuzuia mzozo wa Darfur


Serikali ya Sudan imesema Libya imekubali kuzuia vitendo vya waasi katika eneo la Darfur.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Kamal Hassan Ali, amesema nchi hizo mbili zimekubaliana kuwa kiongozi wa kundi la waasi wa Justice and Equality Movement- JEM, Khalil Ibrahim, hataruhusiwa kufanya mashambulio dhidi ya Sudan kutoka ardhi ya Libya.

Amesema Khalil Ibrahim, kwa sasa ametengwa na hana budi ila kurejelea mazungumo ya amani.

Rais wa Sudan Omar al Bashir, amekamilisha ziara rasmi ya siku mbili nchini Libya ambako alifanya mashauriano na kiongoni wa nchi hiyo Muamar Gadaffi.

No comments:

Post a Comment