KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 16, 2010

Katibu Mkuu wa UN azuru Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anazuru Pakistan, ili kujionea maafa yaliyosababishwa na mafuriko, ambapo serikali inasema yamewaathiri watu millioni ishirini.

Bw Ban atazuru baadhi ya maeneo yaliyoathirika vibaya-siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Pakistan, Yusuf Raza Gilani, kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoisahau nchi yake.

Bw Ban atajadiliana na maafisa wa Pakistan jinsi ya kuimarisha shughuli za misaada.

Umoja wa Mataifa hadi sasa ulitoa wito wa kupatiwa dola millioni mia nne na sitini kusaidia waathiriwa.
Pakistan yajitetea


Wakati huo huo serikali ya Pakistani imejitetea kuhusiana na shutma kuwa haikuwafikia watu wengi walioathiriwa na mafuriko yaliyosababisha uharibifu mkubwa nchini.

Waziri wa habari, Samsun Bokhari, alisema serikali inafanya kila iwezalo kuwafikia watu wote milioni ishirini walioathirika.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Yousuf Raza Gilani,alisema atashirikiana kwa karibu na upinzani kukusanya fedha za kusaidia waathirika.

Naye Rais Asif Ali Zardari, amekuwa akiwatembelea baadhi ya watu walioachwa bila makao na mafuriko hayo.

No comments:

Post a Comment