KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, August 25, 2010

JWTZ yatoa hofu wananchi

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tahadhari na kuwataka wananchi kutohofu na hali hiyo kwa kuwa jeshi hilo linatarajia kurusha ndege hewani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Majeshi.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana, na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ jijini Dar es Salaam.Ndege hizo zinatarajiwa kurushwa mfululizo Septemba Mosi mwaka huu, katika kilele cha sikukuu hizo za majeshi nchini.

Taarifa hiyo iliwataka wananchi kuondoa hofu na jambo hilo na wametakwia watulie wakati zoezi hilo likiendelea.

Kilele cha madhimisho hayo yatafanyika Kigamboni ikiwa ni pamoja na kuadhimisha miaka 46 tangu jeshi hilo kuanzishwa kwake mwaka 1964.

Pia jeshi hilo ilitoa fursa ya pekee kwa wananchi waishio Dar es Salaam na kwingineko kuhuhuria maonyesho hayo kuona ni jinsi gani jeshi hilo linafanya kazi zake

No comments:

Post a Comment