KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 30, 2010

Magari 46 Yagongana, Watu 72 Wajeruhiwa

Jumla ya magari 46 yamegongana kwa wakati mmoja nchini Ureno katika ajali mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea nchini humo na kupelekea vifo vya watu 6 na watu 72 kujeruhiwa.
Ajali hiyo mbaya ilihusisha magari toka pande zote mbili za barabara ya A25 iliyopo kusini mashariki mwa mji wa Porto.

Jumla ya magari 46 yaligongana kwa wakati mmoja ambapo malori mawili na magari madogo sita yaliteketea kwa moto.

Watu sita walipoteza maisha yao na wengine 72 walijeruhiwa huku 24 kati yao hali zao zikisemekana kuwa ni mbaya.

Sababu ya kutokea kwa ajali hiyo inasemekana kuwa ni mvua na ukungu

No comments:

Post a Comment