KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Alalamikia tabia za baba mkwe


MSICHANA mmoja jina kapuni [25] mkazi wa Banana jijini Dar es Salaam, amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuchoshwa na vitabia anavyoviita vichafu anavyofanyiwa na baba mkwe wake hali inayomfanya kutamani kuhama ndani ya nyumba hiyo.
Msichana huyo alidai kuwa, baba mkwe wake amekuwa na tabia anazodai ni za utovu wa nidhamu ambazo hazistahili kufanyiwa ikiwa kama mkwe wake na anakwenda kinyume na tamaduni za kitanzania.

Msichana huyo mrembo mfanyakazi wa benki ya NMB amedai anakwazwa na mkwe wake kwa kuonyesha dalili za kumtamani hali inayomfanya akose raha na kuogopa kumwambia mumewe wake, kwa kuwa angeweza kuhatarisha ndoa yake ambayo ni changa.

Alidai kuwa mume wake ambaye pia ni mfanyakazi wa benki hiyo lakini walikuwa katika matawi tofauti ya utumishi, walioana mwishoni mwa mwaka jana.

Alidai kuwa mkwe wake huyo, ambaye ni mwalimu mstaafu alikuja kuishi nyumbani kwake hapo tokea Machi mwaka huu, akitokea mkoani Kilimanjaro na amekuwa akimfanyia vituko vya hapa na pale hali inayomfanya akose raha na nyumba yake.

Alidai kuwa baba huyo mwanzoni kabisa alikuwa akiona mwanae ametoka na kuaga,baba huyo amekuwa akiingia chumbani kwake bila hodi hali iliyoimfaya amshangae na akifanya hivyo hujitetea na kumwambia kuwa amuandalie aidha chakula ama kumuuliza kitu chochote huku yeye akiona yuko sahihi.

Alidai hali hiyo ilijirudia mara mbili hali iliyomfanya akaombe ushauri kwa nduguze huku bila kumdokeza mumewe tabia anazofanya baba yake ya kuingia chumbani kwao.

Alidai baba huyo alikuwa akimfanyia vituko vya aina mara aombe wale chakula kwa pamoja, mara nyingine amsifie kuwa ni mrembo sana, na kupigia simu mara kwa mara akiwa kazini mara nyingine akimuhimiza awahi kurudi kwa kuwa amemkumbuka.

Alidai kuna siku baba huyo alimshika sehemu zake za makalio alijisikiavibaya na kuingia ndani kwenda kumwaga machozi kwa uchungu kutokana na hali hiyo.

" Hofu yangu siku moja huenda atanibaka, simuamini sijui nimwambie mume wangu? alijiuliza

Hivyo dada huyu alikuwa anajaribu kuomba ushauri kwa wasomaji wa mtandao huu afanyeje kutokana na taiba za baba huyo kabla hajamwambia mumewe.

No comments:

Post a Comment