KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 30, 2010

Wafanyakazi zaidi kugoma Afrika Kusini


Maelfu ya wafanyakazi wa viwanda vya kutengeneza magurudumu ya gari na wale wa secta ya maji, leo wanatarajiwa kujiunga na wafanyakazi wengine wa umma wanaogoma kuhusu nyongesa ya mishahara.

Shinikizo dhidi ya utawala wa rais Zuma bado zinaendelea kutolewa, huku mgomo huo ukiingia wiki yake ya tatu. Shule zimefungwa na hospitali nyingi hazina wahudumu wa kutosha.

Wafanyakazi wa umma wakiwemo waalimu na wauguzi wanataka nyongesa ya 8.6%, kiasi ambacho ni asilimia mia moja ya mfumuko wa bei nchini humo.

Chama cha muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini, COSATU, kimewataka wafanyikazi wa sekta ya kibinafsi kujiunga nao katika mgomo huo siku ya alhamisi wiki hii ikiwa matakwa yao hayatakuwa yametekelezwa.

No comments:

Post a Comment