KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Aomba talaka kinguvu,ili aolewe na mwingine


HUKU wengine wakiomba kila kukicha wapate wenzi wao wafunge pingu za maisha waishi kwa raha mustarehe,mwanamke mmoja alitoa kioja baada ya kudai talaka kinguvu huku jamii iliyomzunguka ikimshangaa kwa kilichosemekana amepata mwanaume mwenye fedha
NIFAHAMISHE ilishuhudia mwanamke huyo, alipokuja kwa wifi yake,kumueleleza akamwambie kaka yake ampe talaka kwa kuwa alichoshwa na tabia zake,na kumuamuru akiwa hajampa talaka hiyo ataondoka hata kama hajatekeleza.

“Mimi namuomba talaka kaka yako hataki kunipa ana maana gani? mimi simuhitaji tena nimechoshwa na dhiki mimi, anipe karatasi langu niondoke nyumbani kwake” na asiponipa naenda bakwata lazima aitoe” alifoka dada huyo kwa sauti bila hata chembe ya aibu

Wifi huyo alijaribu kumueleza alikosewa nini na kaka yake huyo, na swali hilo hakutaka kulijibu na kumueleza kuwa yeye anachohitaji ni talaka hahitaji maswali,

Hata hivyo mwanamke huyo ilifahamika na ndugu zake kuwa,alikuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwingine ambaye alimuona atambadilisha kimaisha kwa kuwa ndugu zake hao alidai mwanaume huyo alikuwa na fedha zaidi ya mume wake wa sasa.

No comments:

Post a Comment