KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Jua Lachomoza Malawi


Malawi imebadilisha bendera yake na kuiondoa alama ya jua linalochomoza iliyowekwa enzi za ukoloni na kuliweka jua kamili.
Jua linachomoza asubuhi katika bendera ya Malawi, limeondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na jua lilitokeza kamili.

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika akiongelea sababu ya kubadili bendera ya nchi hiyo alisema "Tuko mwaka 2010 nchi yetu imebadilika sana hatuwezi kuwa kama tupo mwaka 1964", alisema rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika.

Alama hiyo ya jua katika bendera ya Malawi yenye rangi za kijani, nyeusi na nyekundu iliwekwa mwaka 1964 na Waingereza baada ya Malawi kupewa uhuru wake.

Kubadilishwa kwa bendera ya Malawi kumepokelewa kwa mitazamo tofauti baadhi ya watu wakisema kuwa hakukuwa na umuhimu wa kuibadilisha bendera hiyo.

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi, Kennedy Makwagwala aliponda uamuzi wa kuibadili bendera hiyo kwa kusema "Hakuna umuhimu wa kubadilisha bendera, hakuna lolote lililobadilika, wananchi bado wanaishi maisha ya dhiki".

No comments:

Post a Comment