KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, August 4, 2010

Amani yahimizwa wakati wa kura ya maoni Kenya


Amani yahimizwa wakati wa kura ya maoni Kenya

Wapiga kura nchini Kenya hii leo wanaipigia kura ya maoni rasimu ya katiba mpya, ombi la amani likitolewa na viongozi kote nchini humo.
Kura hii ya maoni inafanyika miaka miwili baada ya mamia ya watu kuuawa katika ghasia zilizozuka punde baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Katiba mpya imelenga kubadilisha mfumo wa siasa za Kenya na kuzuia kutokea tena kwa ghasia hizo zilizowaacha maelfu ya watu bila makao.

Kura ya maoni imeonyesha kuwa katiba hiyo itakubaliwa na wanachi.
Wanaoiunga mkono katiba wanasema kuwa itachangia ugawanaji wa mamlaka kwa kuunda utawala wa majimbo, kumaliza ukabila na pia kusuluhisha au kuleta mabadiliko katika sera ya ardhi.


















miongoni mwa viongozi waliotoa wito wa amani wakti wa shughuli hiyo ni rais Mwai Kibaki, waziri mkuu Raila Odinga na viongozi wa tyme ya muda wa uchaguzi nchini humo. IIEC.

No comments:

Post a Comment