KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 2, 2010

Alicia Keys afunga ndoa na Swizz Beatz

Alicia Keys ameolewa na mtayarishaji wa muziki Swizz Beatz, ambaye ana ujauzito wake, katika hafla iliyofanyika kwa faragha mwishoni mwa wiki.

Wapenzi hao walifunga ndoa siku ya Jumamosi katika eneo moja ambalo halikutangazwa hadharani.

Mwakilishi mmoja wa Keys alithibitisha kufanyika kwa sherehe hiyo ya harusi kwa shirika la habari la AP siku ya Jumapili.

Mwanamziki huyo aliyewahi kushindi tuzo za Grammys na Swizz Beatz- ambaye jina lake halisi ni Kasseem Dean- wamekuwa pamoja tangu mwaka 2008.

Keys, mwenye umri wa miaka 29, ameshinda tuzo 12 za Grammys tangu kutoa albamu yake ya kwanza Songs in A Minor mwaka 2001.

Dean, mwenye umri wa miaka 31, ambaye ana watoto wawili kutoka ndoa yake ya mwanzo, ameandika na kutayarisha nyimbo za wasanii zilizovuma sana akiwemo Beyonce na mumewe Jay-Z.

Key aliimba katika sherehe za ufunguzi za Kombe la Dunia mwezi Juni.

No comments:

Post a Comment