KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 2, 2010

Agathon Rwasa aondolewa kinara wa FNL

Mzozo a kisiasa unaendelea kutokota nchini Burundi huku taarifa za hivi punde zikiarifu kuwa kiongozi wa FNL Agathon Rwasa ameondolewa mamlakani.

Kundi moja la chama hicho limefanya kikao maalum ambapo Emmanuel Mibiro aliyekihama FNL na kujiunga na serikali aliteuliwa kiongozi . Mibiro kwa sasa anahudumu kama mshauri wa Rais Nkurunziza. Jacques Bigirimana ameteuliwa katibu Mkuu.

Hata hivyo washirika wa Rwasa wamepuzilia mkutano huo na kuutaja kama njama za serikali kukisambaratisha chama cha FNL. Makamu mwenyekiti,Alfred Bagaya amesema Agathon Rwasa ndiye kinara wa chama cha FNL na kamba hakuna kinara mwingine anayetambuliwa na wanachama.

Kundi lililomtimua Rwasa limesema kuchukua hatua hiyo baada yake kutorokea mafichoni na hivyo kuhujumu shughuli za chama hasa pale alipotangaza chama hicho kususia uchaguzi mkuu Burundi.

Agathon Rwasa ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa rais Pierre Nkurunziza katika uchaguzi mkuu wa mwezi Juni.

Hata hivyo aliongoza vyama vikuu vya upinzani kususia uchaguzi huo akilalamikia dosari kwenye mfumo wa uchaguzi. Kwa sasa Rwasa yupo mafichoni akihofia usalama wake.

Na kufuatia tukio la jana, kuna hofu ya kuzuka upya kwa vita.

No comments:

Post a Comment