KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 23, 2010

Mwkalebela na mkewe kizimbani


ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, na mkewe, Selina Mwakalebela wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya mkoa wa Iringa wakikabiliwa na mashitaka ya kutoa rushwa.
Washitakwia hao walifikishwa mahakamani hapo na Takukuru wakikabiliwa na mashitaka hayo ambayo waliyatenda katika mchakato wa kura za maoni ambapo Mwakalebela alikuwa akiwania kiti cha ubunge jimbo la Iringa Mjini.

Washitakiwa hao walifiksihwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Gladys Barthy, na kusomewa mashitaka na Prisca Mpeka na Imani Mizizi ambao ni waendesha mashitaka wa Takukuru,

Walidai kuwa, washitakiwa hao wote kwa pamoja walitoa hongo ya Sh. 100,000 kwa mjumbe aliyetambulika kwa jina la Gwido Sanga, ili aweze kuwagawia wajumbe wengine katika kikao cha kura za maoni..

Hata hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka na kuachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo Mahakama iliwataka kuwa na wadhamani wawili kila mmoja ambapo mmoja lazima awe mtumishi wa serikali na kuwasilisha hati isiyohamishika mahakamani.


Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment