KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 21, 2010

Xenophobia - SA - Jeshi latumwa kusaidia


Jeshi la Afrika Kusini limeungana na Polisi, kushika doria mjini Johannesburg kufuatia mashambulio ya chuki dhidi ya wageni yaliyowaacha watu 7 na majeruhi mabaya.

Miongoni mwa waliojeruhiwa na wahamiaji kutoka Zimababwe na Msumbiji, pamoja na waafrika weusi wa Afrika Kusini waliojikuta katika mashambulio hayo jana usiku.

Katika barua kwa rais Jacob Zuma, mkuu wa chama cha Democratic Alliance upande wa Western Cape Hellen Nzila ameelezea chimbuko la chuki dhidi ya wahamiaji weusi au Xenophobia. Hata hivyo hofu yake ilipuuzwa na mkuu wa polisi kama iliyokosa msingi.

Lakini sasa hivi imebainika wazi kuwa wageni kutoka Zimbabwe Msumbiji, Malawi na Nigeria, miongoni mwa nchi nyingine wanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa wakati wowote.

Tangu mashindano ya Kombe la dunia kuisha nchini Afrika Kusini, wageni wasiopungua 10 wameuawa na watu weusi wa Afrika kusini katika sehemu ya Cape Town na hatari hii imeanza kuenea katika miji mingine.

Mkuu wa Polisi Mbeki T'wele ameahidi kuongeza idadi ya polisi wa kushika doria mitaani, kuimarisha uslama.

No comments:

Post a Comment