KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 21, 2010

Amani ya Sudan kujadiliwa na kikao cha AU


Wajumbe wa Umoja wa Afrika, leo wanatarajia kujadili ripoti inayoelezea hatma ya Sudan baada ya kura ya maoni kuhusu kujitawala kwa eneo la kusini hapo mwakani.

Ripoti hiyo ya kundi la mashirika ya jamii lijulukanlo kama Darfur Consortium inaelezea hofu kuwa mizozo inayoshudiwa kote nchini humo inatishia amani Afrika nzima.

Kundi hilo linataka wajumbe wa Umoja wa Afrika wanaokutana mjini Kampala washughulikie suala hili la Sudan kwa makini.

Mkuu wa shirika la Darfur Consortium Dismas Nkunda ameambia BBC kwamba wanapendekeza kuongezwa walinda amani zaidi pamoja na kupewa nguvu kuzima makabiliano yanayozuka na kutishia maisha ya wakimbizi walioko kambini.

Nkunda pia ameelezea wasi wasi kwamba kura ya maoni ya kuamua uhuru wa Sudan Kusini haiyafanyiwa maandalizi mufaka, hali inayotishia kuzuka kwa vita.

Darfur Consortium imeonya kuzuka kwa vita kote nchini Sudan ikiwa hali ya sasa haitaangaziwa. Aidha shirika hilo linasema kudidimia kwa hali ya usalama nchini Sudan kunatishia uthabiti kwa bara nzima la Afrika.

No comments:

Post a Comment