KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

WFP kununua chakula kutoka Afrika


Shirika la chakula duniani WFP, linasema linajitahidi kuongeza kiwango cha chakula, ambacho huwa linanunua, kutoka kwa wakulima barani Afrika.

Mkuu wa shirika hilo Josette Sheeran, amesema wanajitahidi kuhakikisha kuwa nchi kumi na sita kutoka barani Afrika, zitafaidika kutokana na mpango huo.

Katika nchi nyingi barani Afrika, wakati kuna uhaba wa chakula mashirika ya misaada ya kimataifa huanza kuleta chakula ambacho hununuliwa katika nchi za kigeni.

Hili ndilo tatizo ambalo shirika la WFP linajaribu kumaliza.

Uganda ni moja wapo ya nchi ambazo shirika hilo lina mpango wa kununua chakula.

Mkrugenzi wa WFP nchini Uganda Stanlake Samkange, amesema fedha nyingi zitatumika kununua vifaa vitakavyoliwezesha shirika hilo, kununua kiwango kikubwa zaidi mahindi na maharage.

Vifaa hivyo vitatumika kuhifadhi na kusafisha chakula hicho, ili kiweze kufikia kiwango cha kimataifa.

Mwaka jana Shirika la WFP, lilitumia dola millioni mia mbili na ishirini kutoka barani Afrika.

Wakulima kutoka Uganda, ni baadhi ya wale waliofaidika.

Hii ina maana kwamba maharage waliyopewa watu wa Karamoja,kaskazini mashariki mwa Uganda yalinunuliwa kutoka Kusini-Magharibi mwa Uganda, na wala sio kutoka mashamba ya Marekani au Ulaya.

No comments:

Post a Comment